Msanii kutoka katika kundi la TMK Mheshimiwa Temba azungumzia wazo la kuanzishwa kwa kundi la ”Mkubwa na Wanae” lililopo chini ya meneja Saidi Fella.
Akizungumza na Enewz Temba amesema kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo kwa Fella la kuanzishwa kwa kundi hilo baada ya baadhi ya wasanii waliokuwa chini yake kulaumu kudhurumiwa na meneja huyo.
“Mimi nilimuuliza bosi Fella kwa nini kila siku unalaumiwa kuwadhurumu wasanii lakini hao wasanii hawazungumzi kabla ya wao kupata mafanikio walitokea wapi ndomana nikamwambia tuanzishe mkubwa na wanae, tumeanzisha kundi la Mkubwa na Wanae; mimi, Fella na Chambuso kwaajili ya kuwasaidia watu kufika katika matumaini ambayo wapo nayo sasa”, alisema Temba.
eatv.tv
Comments
comments