Thea Adaiwa Kuhongwa Gari
STAA wa filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ sasa hivi anasukuma mkoko baada ya kutembea kwenye vumbi kwa muda mrefu lakini pia taarifa zilizo nyuma ya pazia zinadai eti kahongwa na mwanaume.
Inadaiwa baada ya Thea kumwagana na Michael Sangu, alijiweka kwa mwanaume mwenye nazo na ndiye aliyempa jeuri ya kumiliki gari hilo aina ya Toyota Passo.
“Thea sasa mambo safi, anatembelea makalio baada ya kuhongwa gari na yule bwana wake wa sasa,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kunyaka ‘ubuyu’ huo, Thea alitafutwa, alipopatikana alisema: “Hili gari sijahongwa na katika maisha yangu sitegemei kuhongwa na mtu yeyote, nimenunua kwa hela yangu ninayopata kwenye muvi.”
Chanzo: GPL