MSANII mkongwe wa fi lamu Bongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amejikuta akitetwa akidaiwa kuwa mcharuko kwa kuvaa vimini hasa baada ya kuachana na mumewe, Michael Sangu ‘Mike’.
Kutetwa huko kumeonekana kumkera sana Thea ambaye juzikati akichonga na Ijumaa alisema, anawashangaa wanaomsema vibaya kwani anaamini anaishi maisha anayotaka yeye na wala hakuna anayeweza kumzuia.
“Mimi napenda kuvaa vimini tangu zamani na sasa hakuna anayenizuia kwani haya ni maisha yangu, nawashangaa sana anaonisengenya yaani wananikera sana sijui ananitafuta nini, siwezi kuwa mcharuko kwa sababu eti ndoa imevunjika ama wanavyosema kwa sababu mimi ndiye niliyemuacha Mike hivyo wanikome,” alisema Thea.
Chanzo:GPL
Comments
comments