Msanii wa muziki wa bongo fleva Timbulo amefunguka na kusema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wamezoea kupata kidogo katika maisha yao ya kila siku ndiyo maana inapotokea wamepata kikubwa wanawehuka na kuvurugika.
Timbulo alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz ya EATV na kusema kuwa kuna baadhi ya wanawake wakipata fedha au mafanikio katika maisha yao wanabadilika na kuwa na mashauzi na kwamba wanajisahau walipotoka na kuanza kuonesha dharau.
“Watoto wa kike wamezoea kupata kidogo wakipata kikubwa wanawehuka, wanabadilika wanajiona wasichana wazuri, na ikishatokea akaanza kuonekana kwenye TV vichwa vyao vina vurugika akili, wanashindwa kutambua nafasi walizopata, mimi naamini ukipata nafasi ya kufanya kazi na msanii yoyote anayefanya vizuri ni nafasi nzuri kwa msanii wa kike na yeye kufanya vizuri” alisema Timbulo
Msanii Timbulo alisema haya baada ya kuzinguliwa na msanii Vanessa Mdee pamoja na Malaika
Eatv.tv
Comments
comments