MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata CD na DVD 650,000 zenye thamani ya Sh bilioni moja kwa ukwepaji wa kodi.
Pia katika zoezi hilo mitambo 47 ya kudurufu CD na DVD pamoja na kompyuta nne zimekamatwa.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema bidhaa hizo zilipatikana baada ya kuwepo kwa msako mkali ulioshirikisha wadau wa tasnia ya muziki na filamu.
Alisema baada ya kukokotoa kupitia gharama ya ushuru wa bidhaa hizo waligundua kuwepo kwa upotevu wa Sh milioni 31 na milioni 11 ambazo zilikuwa ni gharama za stempu zilizotakiwa kubandikwa katika CD na DVD hizo.
“Makampuni yanayoshiriki katika uuzaji wa kazi hizo kinyume na sheria ni Kilimanjaro house music, Oneshop, Siku hazifanani DVD, roommate technology, fety big star wanaofanya kazi hizo eneo la Kariakoo,” alisema Kayombo.
Mtanzania
Comments
comments