Trey Songz Amenipa ‘Kiki’ Hadi Marekani – Vanessa
Msanii wa muziki wa bongo fleva, mwanadada Vanessa Mdee a.k.a Vee Money, amefunguka na kueleza faida alizopata kwa kuwa karibu na nyota wa muziki nchini Marekani Trey Songz.
Akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, Vanessa alitakiwa kueleza faida alizopata kutokana na skendo zilizovuma siku za hivi karibuni kuwa alitoka kimapenzi na Trey Songz kipindi walipokuwa nchini Kenya katika Coke Studio.
Katika majibu yake, Vanessa alisema kuwa hakuna jambo linalovuma kwake bila ya kuwa na faida, na kwamba skendo hizo zilivuma hadi Marekani, kwani aliandikwa katika baadhi ya blogs za Marekani kuhusu ukaribu wake na Trey Songz, kitu kilichomfanya kujulikana hadi katika taifa hilo lenye nguvu katika karibu kila nyanja, ikiwemo muziki duniani.
Katika FNL ya Sam Misago ilikuwa hivi…….
Swali: “Vipi ishu ya wewe na Trey Songz imekupa faida gani, je kuna Wamarekani wamekujua au imeishia hapa hapa?”
Jibu: “Yea, hakuna jambo naweza fanya bila manufaa, hiyo imenifanya niandikwe kwenye blogs kadhaa nchini Marekani, kwahiyo wamarekani wamenijua”
Trey Songz amekuwa akifananishwa kimuonekano na mpenzi wa Vanessa, Jux licha ya Jux mwenye kuweka wazi kuwa Trey Songz ndiye role model wake.
Katika hatua nyingine Vanessa ameeleza furaha yake kuingia kwenye tuzo za EATV, na kuomba mashambiki kumpigia kura katika kipengelee cha Mwanamuziki Bora wa Kike.
eatv.tv