Tunahitaji Ukombozi Kisanaa- Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Wanawake
WENYEKITI wa Chama cha Wanawake wa Tasnia ya Filamu Tanzania (CWTF) Vanitha Omary amesema kuwa baada ya kuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu wamekaa na kutafakari na kuamua kuanzisha chama kinachoshirikisha wasanii wa kike katika kuleta maendeleo na ukombozi kisanaa.
“Sisi kama wasanii wa wanawake jamii inatutegemea katika mambo mengi hivyo lazima tuwe na umoja imara kuleta ukombozi wa kifikra na kujenga tasnia yenye mwelekeo kwa maendeleo zaidi,”alisema Vanitha.
Chama cha CWTF kina uongozi ambao ni mwenyekiti ni Vanitha Omary, Mwenyekiti msaidizi ni Ndumbagwe Misayo, Katibu ni Halima Yahaya ‘Davina’ katibu msaidizi ni Joan Matovolwa, mweka hazina Hellen Luanda na nidhamu Coletha Raymond mwenyekiti anasema milango ipo wazi waigizaji wa kike wanakaribishwa.
Ujio wa chama hiki ni changamoto kwa waigizaji wa kiume ambao wamekuwa ndio nguzo ya tasnia ya filamu kwa kuongoza kuwa na watayarishaji wengi kuliko wanawake lakini hawajakuwa na umoja
FC