Artists News in Tanzania

Tunda Afunguka Kutoa Mimba

Mlimbwende Tunda ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake, amekana taarifa za kutoa ujauzito ambao alionekana nao, na kusema hakuwa na mimba na hajawahi kupata ujauzito maishani mwake.

Akizungumza na mwandishi wa East africa Television Tunda ambaye pia ni ‘video vixen’, amesema tumbo alilonalo lilikuwa ni kitambi kilichoongezeka kutokana na kunenepa, na kwa sasa anafanya mazoezi kuweza kurejesha mwili wake wa kawaida.

“Sina mimba na sijawahi kuwa mjamzito, hili tumbo nimeongezeka tu nina asili ya tumbo nikinenepa na tumbo linaongezeka, hizo tetesi za kutoa mimba ndo nazisikia kwako sijawahi kutoa mimba”, amesema Tunda.

Hivi karibuni mrembo huyo amekuwa akipost picha zinazomuonyesha na tumbo kubwa, hali iliyoibua gumzo kwa mashabiki kuwa huenda mrembo huyo anatarajia kupata mtoto

 

Comments

comments

Exit mobile version