Artists News in Tanzania

Tunda Man Atoa Ushauri Huu kwa Madee Kuhusu Ndoa

Msanii wa bongo fleva Tunda Man amemshauri rafiki yake Madee kufunga ndoa kwa kuwa amemzidi umri na ana mwanamke ambaye anampenda hivyo haoni sababu ya Madee kuacha kufunga ndoa na yupo tayari kuchangia mahari ya Madee.

 

Akiongea ndani ya eNewz Tunda amewapongeza wasanii wezake waliofunga ndoa akiwemo Nyandu Tozi, Mwana Fa , Mabeste na wengine Tunda amewasihi wasanii wenzie wa dini ya kiislamu kufunga ndoa kwa kuwa zitawasaidia kuongeza heshima katika jamii inayowazunguka.

Hata hivyo Tunda amewachana wasanii wanaoongopa kufunga ndoa wakihofia kushuka kwa muziki wao kwamba hawana hofu ya Mungu kwani kupanda na kushuka ni mipango ya Mungu na wapo kina Mr. Blue wamefunga ndoa na bado wanafanya vizuri kimuziki.

Harusi ya Tunda Man

eatv.tv

 

Comments

comments

Exit mobile version