Artists News in Tanzania

Tunda Mapenzi ya Mitandaoni Byebye!

MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Tunda Sebasita ‘Tunda’ hivi karibuni amefunguka kuwa miongoni mwa mambo ambayo hawezi kuyaweka wazi kwa sasa mitandaoni ni juu ya uhusiano wake wa kimapenzi ili kuwaepusha marafiki wenye wivu kumharibia uhusiano wake jambo ambalo lilimtokea kipindi akiwa na Young D.

Tunda Sebasita ‘Tunda’

Akichonga na Uwazi Showbiz, Mwanadada huyo alisema kuwa kipindi yupo na Young D watu wengi walikuwa wanafahamu juu ya uhusiano wake kwa sababu alikuwa muwazi mno kwenye vyombo vya habari jambo ambalo lilisababisha wawe wanaunda maneno mengi kuhusu mpenzi wake huyo ilimradi aachane naye.

“Kiukweli nimejifunza juu ya kuwa muwazi katika suala zima la mapenzi kuwa kuna watu wengine hawapendi kuona mnakuwa na furaha.

“Hawa huweza kupenyeza maneno ya kuwagombanisha ilimradi tu muweze kuachana, sasa mimi nimeamua katika uhusiano wangu wa sasa kutokuwa muwazi, mtu anayefahamu juu ya ninatoka na nani kwa sasa lazima atakuwa amefanya kazi ya ziada,” alimaliza Tunda.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version