Kupitia ukurasa wake wa Instgram Wema aliandika ujumbe ambao umeleta utata kwa baadhi ya mashabiki ambao wanahisi huenda Wema Sepetu bado ana ujauzito kutokana na kitendo chake cha kutotaka kupost picha zake mpya na kutokana na mabadiliko yake ambayo wanahisi yanaletwa na ujauzito. Ingawa mashabiki wengine wamekuwa wakimshauri kuwa anapaswa kupunguza mwili wake kwa kufanya mazoezi huku wengine wakizidi kumpa sifa kuwa anazidi kupendeza.
“Ni hii tu naipost sababu nampenda sana Huyu mwanamke… Ila sasahivi sijui nijifungie tu ndani maana zoezi la mpaka ‘June’ ni Kubwa. Haya na msisahau kunipa na ushauri wa dawa gani za kutumia nipungue sio kwa ubonge nilionao sasa. ‘But not my fault’ ni fault ya vile vitwins vyangu vile. Weightloss imekuwa ni ngumu sana kwangu” aliandika Wema Sepetu.
Comments
comments