Tangazo lenye zuio la mahakama la kuzuia uchaguzi huo kwa muda.
UCHAGUZI wa Meya jiji la Dar es Salaam, uliokuwa ufanyike leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, umeahirishwa tena mpaka itakapotangazwa siku nyingine.
Akitangaza kuahirisha uchaguzi huo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo Theresia Mbwambo amesema kuwa, sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo ni kutokana na baadhi ya watu kufungua kesi mahakamani kuzuia uchaguzi huo. Hivyo akasema sababu ni court injuction yaani pingamizi la mahakama.
Baadhi ya wabunge na madiwani kutoka vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamepinga vikali kuahirishwa mara kwa mara uchaguzi huo huku wakiahidi kwenda mahakamani Jumatatu ili kufungua kesi ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, amesema hawakubaliani na sababu zilizotajwa za kuahirisha uchaguzi huo na ksisitiza kuwa watakwenda mahakamani kupinga hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
comments