Uongo Unaangusha Bongo Movie – Patcho Mwamba
MUIGIZAJI wa filamu Bongo Patcho Mwamba amefunguka kuwa tabia ya uongo kwa baadhi ya wasanii wakubwa katika tasnia ya filamu kunakimbiza baadhi ya wawekezaji katika tasnia ya filamu Bongo, kwani wengi si wakweli na udanganya kila mtu kuanzia wao kwa wao hadi matajiri.
“Unaenda location na nguo viatu kibao ili usipate shida ukiondoka unaangalia hakuna kiatu unamuuliza Producer hajaona inapita siku unakutana naye kavaa kiatu chako sasa unashangaa tu,”alisema Patcho.
Msanii huyo wa filamu na muziki anasisitiza kuwa lazima wasanii kuwa na nidhamu na uaminifu ndio silaha ya kujenga imani kwa wadau wengine hata wale wawekezaji wadogo wadogo kwani tasnia ya filamu bado inahitaji uwekezaji mkubwa ili iweze kuwalipa wote wanaoshiriki.
Pia msanii Rais wa Bendi kubwa ya muziki wa Dansi FM Academia anasema kuwa anajivunia filamu ya Bei Kali ambayo bado haijatoka inatarajia kutoka mwezi wa kumi ikisambazwa na kampuni ya Papazii Entertainment itazidi kuonyesha umahiri wake katika kuigiza Bongo msanii namba moja kwa kuvaa pamba kali.