Uwoya Hawezi Kuusahau 2017
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye Bongo Movies, Irene Uwoya amesema kuwa, hawezi kuusahau mwaka uliomalizika jana wa 2017 kutokana na kukumbana na vitu vingi maishani kuliko kipindi kingine chochote.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Uwoya aliweka wazi kuwa, katika maisha ya mwanadamu, lazima kuna mwaka ambao kuna jambo zuri au baya ambalo humtokea mtu hivyo kwa upande wake mwaka uliopita alikumbana na mambo mengi mabaya ikiwemo kumpoteza mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
“Mwaka 2017 umepita, lakini kwangu nilikutana na matukio mengi, mengine ya kufurahisha kidogo na kuumiza sana. Kubwa ni kumpoteza mume wangu, lakini namuomba Mungu Mwaka 2018 uwe wa baraka tele,” alisema Uwoya.
Chanzo;GPL