-->

Uwoya: Sipendi Kudumu na Mpenzi Mmoja

Staa wa filamu mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Irene Uwoya ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuwa, huwa hana mzuka wa kudumu na mpenzi mmoja kwa muda mrefu akidai kuwa, wakizoeana sana inakuwa kero kwake.

IRENE UWOYA34

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Uwoya alisema kuwa haoni sababu ya kukaa muda mrefu na mpenzi kwa sababu siyo baba yake wala mama yake na anapoamua kuchukua uamuzi wa kumuacha wala haumiagi.

“Yaani mimi kukaa muda na mwanaume sipendagi kabisa na sina mzuka huo kweli. Ndiyo maana mtu nikiamua kumbwaga anahaha na wengine watabembeleza weee lakini wala sina tabia ya kurudi nyuma, kwa kifupi sipendi kudumu na mpenzi,” alisema Uwoya aliyewahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume mbalimbali kabla ya kuolewa na msakata kabumbu raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ambapo ndoa yao haikudumu.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364