Vanessa Mdee Afunguka Kuvunjwa Moyo
Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amefunguka na kudai anamshukuru Mungu kwa kupokelewa vizuri albamu ya ‘Money Monday’ mpaka sasa japokuwa kuna baadhi ya watu wanataka kumvunja moyo.
Vanessa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha ‘FRIDAY NIGHT LIVE’ (FNL) kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na Bill Sepenga kuhusiana na mauzo ya albamu kama yanaenda vizuri au laa.
“Mauzo yanaenda sana kusema ukweli yani nimestaajabishwa sana na mauzo ya albamu, nimefurahi kuona watu wapo teyari kupokea albamu. ‘Is fun’ kuona watu wengine wanataka kunivunja moyo. Mimi naenda baa nauza ‘CD’ mwenyewe wengine wananifukuza wananiambia albamu zimepitwa na wakati”, amesema Vannessa.
Kwa upande mwingine, Vmoney amesema anawashukuru watu wote wanaondelea kumpa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine katika kununua albamu yake ya kwanza kwa mwaka 2018.