Vanessa Mdee Afunguka Sababu ya Kung’ara Kimataifa Kuliko Wasanii Wengine wa Kike wa Kibongo
Staa wa Bongo Fleva,Vanessa Mdee ‘V Money’ amefunguka sababu za kung’ara kwa mziki wake na kubahatika kupata tuzo kadhaa za Kimataifa kuliko wasanii wengine wa kike wa Kibongo.
“Ujue kuna tuzo zingine zinatofautiana kuna zingine wapo wasanii wa Kitanzania ambao tuzo fulani wametajwa, na zingine hawakubahatika kuwepo,ukweli ni kuwa wale wanaoandaa tuzo pia wanaangalia ni msanii gani anafahamika zaidi kutoka nchi fulani yaani msanii anakuwa anajiuza mwenyewe zaidi Kimataifa,’’Alisema Vanessa Mdee.
“Pia baadhi ya wasanii wa Kitanzania ambao wametajwa kwenye tuzo pengine wamepata soko(mashabiki) na nafasi ya kuafahamika zaidi kwenye nchi ambayo imetoa tuzo hizo,”alisema Vanessa Mdee.
Cloudsfm.com