-->

Video: Chid Benz afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Rehab ‘Stay away from Drugs’

Rapa Chid Benz amefunguka kwa mara ya kwanza tangia atoke Rehab alikokuwa akipata matibabu ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na amewaasa vijana watu,iaji wa Tanzania kuacha kabisa mchezo huo.

Rapa Chid Benz

Chid Benz ambaye anaonekana mwenye afya na uso wenye furaha, amesema madawa ya kulevya sio ya kuyazungumzia. Amesema kama mtu hataki kujutia maisha yake yote basi aachane na mchezo huo mara moja.

Stay away from Drugs,wakae mbali sana na madawa ya kulevya kitu kibaya sana sitaki kuongelea sana lakini wajitahidi (Watanzania) kadri wanavyoweza wakae mbali na madawa ya kulevya ni kitu kibaya sana kinaweza kukufanya ujutie maisha yako yote“Alisema Chid Benz kwenye mahojiano yake na Muungwana TV.

Tazama hapa chini mahojiano yake yote.

Chid Benz alishawahi kuathirika na madawa ya kulevya na kupelekwa Rehab mara tatu kabla ya Afya yake kutengamaa.

By Godfrey Mgallah

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364