VIDEO: Irene Uwoya Ataja Kilichomkosesha Ubunge CCM
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefafanua sababu za kutopitishwa na chama chake cha CCM kuwa mbunge wa Viti Maalum vya wanawake, na kusema kuwa kilichomuangusha ilikuwa ni kura za Rais kuwa chache.
Uwoya alikuwa akijibu maswali ya wapenzi na mashabiki zake LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, ambapo swali la kwanza kabisa kuulizwa, lilihoji sababu za yeye kutemwa kwenye ubunge ndani ya CCM na kama bado ana ndoto za kuwa mbunge.
Katika majibu yake, Uwoya alisema bado ana ndoto za kuwa mbunge huku akiweka wazi kuwa yeye hakutemwa na wala hakushindwa katika kinyang’anyiro hicho isipokuwa nafasi yake kuwa mbunge ilikuwa inategemea idadi ya kura ambazo angepata aliyekuwa mgombea urais
“Niligombea kupitia upande wa vijana na nilishinda, sikushindwa wala sikutemwa, kwanza kwa mkoa wa wangu wa Tabora nilipata kura za kutosha tena nilikuwa namba moja kabisa, kwenye taifa pia nilifanikiwa kuwa kwenye majina 10 ambayo yalikuwa yanategea kura Rais, kama Rais angepata kura nyingi basi tungechukuliwa wote, lakini kwa kura alizopata Rais ilibidi wachukuliwe 6, kwahiyo mimi sikushindwa, mimi nilishinda lakini asilimia za kura za Rais ndiyo hazikutosha”. Alisema Uwoya
Kuhusu nafasi ambayo angependa kuteuliwa kwa sasa katika serikali ya awamu ya tano, Uwoya amesema Mungu ndiye anayejua, na wakati ukifika anaweza kupata nafasi yoyote kwahiyo hawezi kujipangia.
Huyu hapa Uwoya akifafanua…..