Staa mkongwe wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ mwishoni mwa mwaka uliyopita alitembelea kituo cha Watoto Yatima cha Msimbazi Centre kilichopo Ilala na kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki msanii huyo amesema anasikia faraja kuwatembelea watoto hao.
JB pia alitumia nafasi hiyo kwa kuongea na uongozi wa kituo hicho kisha kuwatambulisha wasanii walioshiriki katika filamu ya Chungu cha Tatu ambayo imeingia leo sokoni na aliongozana nao walikuwa ni Patcho Mwamba, Bi. Hindu, Mau Fundi, Steven Almas.
Comments
comments