Msanii wa bongo fleva Kassim Mganga amefunguka kwa kusema hajachukizwa na maneno aliyotupiwa na mashabiki zake baada ya kubadili muonekano wake kwa kuwa ni jambo alilokuwa analitegemea tangu awali.
Kassim amesema mashabiki zake wamechukizwa na muonekano wake mpya aliokuja nao huku wengine wakimwambia kwamba muziki anaoufanya na jinsi alivyopaka ndevu rangi havifanani kabisa.
“Unajua unapofanya jambo lazima utegemee ‘Yes na No’ kwa hiyo mimi nilikuwa nategemea tu, haijanistua. Siku ‘plan’ kufanya hivi mimi nimeamka nimejisikia tu kuweka ndevu zangu kuwa na mvi kwa sababu nimeshawahi hina pia ndevu zilikuwa nyekundu ramadhani ya mwaka jana kwa hiyo nikisijisikia naweza nikaendelea au nikaacha pia” alisema Kassim
Comments
comments