Dar es Salaam.Ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imemtaka mmiliki wa Quality Plaza, Yusufu Manji kuripoti uhamiaji mara baada ya kutoka hospitali alikolazwa.
Ofisa uhamiaji wa mkoa huo, John Msumule ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Manji anatakiwa kufanya hivyo kwa kudaiwa kuwa ameajiri watu wanaoishi nchini kinyume cha sheria.