Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii waliofika hapa Oysterbay polisi jijini Dar es salaam kumsubiria rafiki yake Roma Mkatoliki ambaye anahojiwa na jeshi la polisi muda mchache baada ya kupatikana.
Rappa huyo alitekwa Alhamisi iliyopita akiwa studio pamoja na wenzake watatu.
Akiongea na Bongo5 jioni hii akiwa Oysterbay polisi, Nay amesema anashukuru Mungu kupatikana kwa wasanii hao kwani ni tukio ambalo lilikuwa linawaumiza kichwa.
“Nimepata nguvu sana baada ya kusikia mwenzangu wamefika hapa baada ya kupatikana, mimi naamini polisi ni sehemu salama, kwahiyo binafsi nimepata hata nguvu ya kula, hili ni jambo la heri kwa kila mtanzania anayependa muziki,” alisema Nay wa Mitego.
Roma na wenzake bado wanahojiwa Oysterbay polisi.
Comments
comments