Msanii wa filamu za vichekesho Salma Jabu aka Nisha, amefunguka na kuweka wazi kuwa saizi amemsamehe msanii wa muziki wa bongo fleva Baraka The Prince ambaye aliachana naye mwaka jana na kutokea kumchukia sana.
Nisha amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kudai saizi ameamua kumsamehe kabisa kutoka moyoni mwake na kusema ameanza kuwa shabiki mzuri wa kazi zake, tofauti na ilivyokuwa awali baada ya kuachana kwani alitokea kumchukia sana hata kazi zake za muziki alikuwa hasikilizi wala kutazama.
Tazama video hii kufahamu mengi zaidi
Comments
comments