Video: Rais Magufuli Awasili Mkoani Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya wafanyakazi ‘Mei Mosi’.
Ijumaa hii Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli pamoja na kushiriki sherehe hizo.