DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wasanii maarufu hapa nchini wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Makonda amewataja askari hao wakati akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam.
RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi.
“Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata.”
“Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya Dar es Salaam natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe.”
“Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya Dar es Salaam maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari.”
“Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya,” alisema RC Makonda.
Comments
comments