Ikiwa ni siku chache toka Ex wa Shilole, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo ‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake huyo, Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.
Nuh amethibitisha kwamba Shilole ndiye aliyemuimbia kwenye wimbo huo, kwa kumtumia video queen anayefanana na Shilole kama pacha katika video ya wimbo huo.
Sholole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe instagram ambao baadae aliutoa:
Wale unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitengo. Umemiss mkong’oto?. Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha… Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako. Nikifungua mdomo wangu utadhalilik
Shilole na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa alizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo, huku Shilole akitaa kuzungumzia kilichotokea.
Bongo5
FANYA BISHARA YA KUUZA FILAMU KUTOKA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT
PIGA NAMBA HIZI: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA
Comments
comments