Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya amefunguka na kutaka siasa isiingizwe kwenye vita ya madawa ya kulevya na kusema viongozi wasimdanganye Rais Magufuli ili kujihakikishia vyeo vyao au nafasi zao katika uongozi.
Ester Bulaya ametoa rai hiyo leo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa taarifa za kamati na kusema Rais anapaswa kuambiwa ukweli ili waweze kumsaidia kupambambana vyema na madawa ya kulevya.
“Tusifanye siasa kwenye vita hii ya madawa ya kulevya, tusimuongopee Rais kwa kutaka kuhakikisha vyeo vyetu tumwambie ukweli, ili kumsaidia Rais anapaswa kumteua kamishina wa hii tume maana tangu tulipopitisha sheria hiki chombo hakina kamishna, tutakapo hakikisha hicho chombo kinapata kamishna kwa kumsaidia Mhe. Rais tutakamata wale wanaoingiza dawa za kulevya wale mapapa na si hao wanaokamatwa sasa hivi” alisema Bulaya
Mbali na hilo Mbunge Ester Bulaya amesema kuwa hawa watu wanaokamatwa saizi wanapaswa kupelekwa mahospitali kupata matibabu na si vinginevyo kwani hao ni waathirika wa dawa.
“Mdogo wangu Makonda akitaka kupambana na dawa za kulevya aende magerezani akakutana na kina mama Reyla watamwambia mapapa wa madawa ya kulevya, ili tuungane pamoja na tunamkaribisha katika hili lindi kuhakikisha nchi yetu inapambana vikali dhidi ya madawa ya kulevya, kwa sababu mimi mwenyewe nina mdogo wangu anayenifuata yupo Mwananyamala anakunywa dawa methadone, hivyo ninachokisema nina uchungu nacho kwa kuwa nimekifanyia utafiti wa kina” Ester Bulaya
Comments
comments