-->

VIDEO:Sina Mpinzani Kwenye Game-Chemical

Rapa wa kike bongo anayesumbua na ngoma ya ‘Queen of Dar es salaam, Chemical amejinadi kuwa hakuna rapa wa kike aliyepo kwenye game mwenye uwezo wa kushindana naye kwa upande wa kuandika mashairi.

Chemical amefunguka hayo kwenye eNewz ya EATV leo na kudai kuwa anaamini yeye ni bora katika ‘game’ hivyo watu wasipende kumfananisha na watoto wadogo ambao bado wanafanya kazi kwa kukopi watu wengine bali wanatakiwa watengeneze utambulisho ili wafike alipo yeye.

“Mimi navyofanya muziki najua Focus yangu, nataka nini, na naelekea wapi, hivyo wamekuja wengi wakaniacha wengine wameshindwa kufurukuta inaonesha jinsi nilivyo na uwezo, i am better unajua ndio maana ni Queen of Dar es salaam. Hao ninaoshindanishwa nao tushindane kwenye vingine lakini siyo kwenye uandishi” alisema Chemical.

Aidha Chemical amedai kuwa hana haja ya kupewa albamu nzima ya rapa mwenzake ‘Rosa – Ree’ ili aweze kuamini kuwa ni mkali kwani tayari amekwisha sikiliza nyimbo zake mbili na anajua jinsi alivyo hivyo yeye bado ni zaidi  kwa ubora.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364