VIDEO:Mzee wa Upako Achumbua Wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa, Awapasomo Alikiba na Diamond
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ ameichambua ngoma wa msanii wa bongo fleva, Darassa inayokwenda kwa jina la Muziki, na kusema kuwa msanii huyo ameimba vitu vya maana sana kwenye ngoma hiyo.
Mchungaji Lusekelo ambaye amewahi kunukuliwa akitumia maneno ya wimbo huo na nyingine kadhaa za bongo fleva katika mahubiri yake, alikumbana na maswali katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, ambapo watu walitaka kujua ni kwanini anatumia muziki wa kidunia katika mahubiri yake, badala ya nyimbo za injili.
Akijibu maswali hayo, Mzee wa Upako amesema yeye kama mwanajamii, anaishi duniani pamoja na wana jamii wengine, hivyo ni lazima ajue matatizo yanayowazunguka watu wake ili aweze kuwasaidia na ndiyo maana anajaribu kufuatilia mambo yanayopendwa na watanzanie ikiwemo muziki wa kidunia.
“Muziki ni muziki, hakuna wa kanisani wala duaniani, cha msingi ni ujumbe tu… Sasa ukisema wacha maneno weka muziki, kuna shida shida gani? Ule muziki mi naupenda sana, anasema hakuna jambo gumu kama kumfundisha chizi, na pia ni ujinga sana kusubiri embe chini ya mnazi. Mimi nina nyimbo nyingi hata za kihindi nasikilizaga sana” Alisema
Mbali na ngoma ya Darassa, pia ametoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kuimba wimbo wa Navy Kenzo unaokwenda kwa jina la ‘Kamatia Chini’, huku akishauri wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo zenye mafunzo badala ya nyimbo za mapenzi pekee.
“Wasiimbe nyimbo za mapenzi tu, walipe pia sadaka kwa taifa… wakati mwingine waimbe na nyimbo ambazo zinaasa maadili”
Kuhusu Diamond na Alikiba, Mzee wa Upako amesita kusema ni yupi anayemkubali zaidi, na kusema kuwa wote ni wa Mungu, na vipaji vyao vimetoka kwa Mungu.
Huyu hapa Mzee wa Upako, akiimba ngoma ya Muziki, Kamatia chini, pamoja na nyimbo kadhaa za zamani