-->

VIDEO:Roma asimulia Walivyotekwa


Msanii Roma Mkatoliki amesimulia kilichomkuta siku ya Jumatano wiki iliyopita huku akieleza kusikitishwa na maneno yanaayoenezwa kuwa yeye na wenzake wamepewa pesa na viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kutengeneza ‘kiki’ kwa maslahi yao binafsi.

Akizungumza leo na wanahabari ikiwa ni siku ya pili baada ya kuachiwa huru baada ya kutekwa kwa takriban siku tatu, Roma amesema kuwa watu wake wa karibu ndiyo wanaosambaza taarifa hizo za uongo wakiwemo wasanii wanaowaambia wananchi kuwa wametumia nguvu zao bure kupaza sauti kwa kuwa wao wamelipwa kufanya kazi hiyo.

“Kuna wasanii wanadai nimeli[pwa dola 5000  huu ni upuuzi. Sisi ni masikini sana maisha yetu ni ya kawaida tu , tunarudije kwa jamii ikiwa tayari wanaambiwa hii ni kiki jamii itatuchukuliaje wakati wao ndiyo walipaza sauti hatimaye tukaachiwa kuwa huru Career zetu zinachukuliwaje ni kitu ambacho kimetuliza sana. Hatuwezi kufanya hivyo mimi pamoja na wadogo zangu hatuwezi ku-risk maisha yetu kwa staili hiyo. Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya” Amesema Roma huku akiugulia maumivu.

Katika mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Roma amedai kuwa hawana uhakika na usalama wa maisha yao kwa sasa kutokana na kuwa tukio liliwakuta wakiwa eneo salama ambalo limezungukwa na ulinzi wa kutosha, jambo ambalo hata baada ya kuachiwa kutoka walipokuwa wakipewa mateso, alipiga ishara ya msalaba.

“Nikisema nina hofu nawaza wasanii wengine wanaotafuta riziki halafu hawana ulinzi kama tuliokuwa nao sisi atakuwa na hofu kiasi gani. Naombeni hili jambo liwatie hofu wote. Hata sisi tunahofu labda muda wowote tukio linaweza kutokea tena. Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge. Nawaomba wenye nafasi za kupaza sauti kwenye majukwaa watusaidie kupaza sauti ili matukio haya yakomeshwe” alisema Roma

JINSI ALIVYOTEKWA

Akisimulia jinsi tukio lilivyokuwa, Roma amesema siku ya Jumatano jioni akiwa studio watu wasiofahamika wakiwa na silaha waliwachukua kutoka eneo la studio ya Tongwe Record wakiwa wamewafunga pingu, na kuwaamrisha kuingia kwenye gari, baada ya wao pia kupanda kwenye gari hilo, waliwafunga vitambaa vyeusi machoni na kuwapeleka pasipojulikana na huko ndipo walipokuwa wakiteswa huku wakiwahoji.

Msanii huyo ambaye aliongea kwa niaba ya wengine wote waliokuwa wametekwa amesema baada ya kufanyiwa mahojiano na mateso mfululizo siku ya Ijumaa usiku waliondolewa katika eneo hilo la mateso na kwenda kutupwa eneo la bahari na kuongeza kuwa baada ya kutembea kwa umbali walijikuta wakiwa eneo la Ununio na ndipo walipopata mwanga wa eneo walilokuwepo hata kuwapelekea kuanza kufikiri jinsi ya kupata msaada.

Ameendelea kusimulia kuwa, muda huo ikiwa ni usiku mnene, walipata msaada wa bodaboda ambayo iliwapeleka nyumbani, na kesho yake baada ya kupewa taarifa kuwa shauri lao lilikwishafika polisi, ndipo walipoamua kwenda katika kituo cha polisi Oysterbay

Amesema hawezi kuongea sana kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea tangu kutekwa , kuteswa hadi kuachiwa kwa kuwa kila kitu amekwishakieleza kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya upelelezi, na kwamba hawezi kuyasema kwa sasa kuhofia kuharibu upelelezi.

TUKIO HILI LIWE SOMO

Roma amesema mshikamano uliooneshwa toka siku ya kwanza ya tukio la kutekwa kwao liliposikika liendelee kuwa kama somo kawa jamii kwa kuwa jambo hilo limewafanya watu kushikamana pasipo kujali itikadi za dini, vyama vya kisiasa wala kujali vyeo.

“Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, msitengane tena mbaki kwenye familia moja kwa kufanya hivyo hamtakuwa mmemkomboa akina Moni na Roma bali wengine ambao pia hatujui ni wangapi wanaofanyiwa matukio kama haya na mwishowe tutakuwa tumekomboa taifa zima. Kwa hiki kilichowafanya muungane basi endeleeni kushikamana. Tusitengane tena” Roma

EATV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364