Mwanamuziki wa injili, Upendo Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo Rais Magufuli atamteua.
Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa si kwa ubunge wa kugombea jimboni.
“Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea…. Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba” Amesema Upendo
Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea.
Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge wa kugombea, amesema masharti ya kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya siasa jambo ambalo halipendi.
Jambo lingine amesema mchakato wa kupata ubunge wa kugombea ni mgumu una mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama, jambo ambalo haliwezi na hivyo kusisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa kumkumbuka katika nafasi zake za kutea
Comments
comments