Mahakama ya wilaya ya Ilala imewahukumu vijana wawili sayi kapama na Rigobert Massawe miaka3 jela au kulipa faini ya laki sita kwa kosa la kudurufu na kusambaza kazi za sanaa kinyume na sheria.
Akisomea mashitaka hayo na karani Plasidia Namalla, mbele ya hakimu Adolf Sachore, katika kesi iliyofunguliwa kwa jarada 240/ 2013. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na gari aina ya Sunzuki Escudo T608 DWB wakisambaza na kuuza mzigo huo.
Watuhumiwa hao waliingia hatiani kwa makosa tatu, likiwemo la kusadikiwa, kutenda kosabna kusambaza kazi ya sanaa kinyume na sheria. miongoni mwa filamu walizokutwa nazo ni Hatia, Mwalimu Nyerere, Groly to Ramadhani na mpenzi chokorate.
Comments
comments