MWIGIZAJI wa filamu wa kiume Simon Mwapagata ‘Rado’ ametamba kwa kusema kuwa yeye ndio mpiganaji pekee ambaye anaamini kuwa ataiokoa tasnia ya filamu na kuwa huru kutoka kwa wezi wa kazi zao bila kutegemea msaada kutoka kwa wasanii wenzake wala Serikali kwani vita hiyo ni ngumu na inahitaji uzalendo siyo njaa.
“Filamu ni maisha yetu na tamaduni yetu na si ya msambazaji ambaye anatakiwa atufanye vile anavyotaka, ndio mimi nilisema ni vita vyangu pekee yangu tena nimebadilisha hata jina sasa ni Rado Volcano wale wababaishaji wasubiri ikilipuka,”alisema Rado.
Rado amedai kuwa siku za nyuma alijitoa sana kupigania tasnia hiyo kwa kuwaamini watu lakini akabaini kuwa anatumika na kuwajengea maslahi watu Fulani sasa anapigana kwa ajili ya wasanii wenzake kuwa na maslahi mapana kwa faida ya kizazi chao na si cha mfanyabiara ambaye kesho anaweza kubadilika na kufanya biashara nyingine.
“Naamini siku nitakaporudi Kariakoo wezi wote watakuwa wamefunga maduka na kuendelea na biashara nyingine ambazo si za Filamu, kama mtu anauza Boda boda au duka la Madela hiyo ndio kazi yao hii watuachie wenyewe,”
Filamu Central
Comments
comments