Mzee Yusuf ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha E News kinachorushwa na EATV kuhusiana na wakezake kuzozana kwenye mitandao ya kijamii na kama suala hilo haliwezi kumharibia katika tasnia ya muziki hapa nchini.
”Wake zangu hawahusiki na ‘usupastaa’ wangu mimi ni Mfalme na wake zangu wanaweza kuondoka lakini mimi nikabakia na ndiyo maana sipendi kuulizwa masuala ya wake zangu”-Amesema Mzee Yusuf.
Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa taarabu na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
Aidha mzee Yusuf amesema baada ya kuona hali hiyo ameamua kama mume kufuta wake zake kwenye mitandao ya kijamii na hata ikionekana mtu anatumia jina la mke wake ijulikane kwamba wake zake hawahusiki tena.
eatv.tv
Comments
comments