Wanaosema Sina Kazi Wanakosea- Idris Sultan
Mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultan amesema kwamba wanaosema hana kazi na anazurura tuu kwenye mitandao ya kijamii wanakosea kwa sababu yeye ni msanii.
Idris amefunguka hayo alipokuwa akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir katika kipindi cha Mkasi Tv Show kinachotushwa na EATV.
”Mimi ni ‘Celebrity’ na kwangu kuwa kwenye mitandao ya kijamii kwangu ni kazi kwa sababu siwezi kufanya ‘interview’ na vyombo vya habari kila siku”-Amesema Idris.
Aidha Msanii huyo pamoja na mambo mengine amefunguka kwamba bado hajaoa na wala hana mtoto.