Wanaume wa Mitandaoni Wamenipa Somo-Giggy Money
Msanii wa Bongo fleva ambaye jana ameachi wimbo wake unaoitwa ‘Supu’ amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hataki tena wanaume wa mitandaoni na kudai kuwa wanaume hao wamempa somo.
Giggy Money akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo amesema kuwa msanii Hemedy Phd pamoja na Rich Mavoko ndiyo wasanii ambao walimtokea kupitia njia ya mtandao na kitu walichomfanya kimemfanya asitamani tena wanaume kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa sasa sitaki kabisa wanaume kwenye mitandao ya kijamii kwani niliwahi kuwa nao wawili ambao walinitokea kwa njia ya mtandao ambao ni Hemedy Phd pamoja na Rich Mavoko ila kwa walichonitenda sitaki tena wanaume wa mitandao ya kijamii,” alisema Giggy Money.
Mbali na hilo Giggy Money amesema kuwa anatamani kufanya kazi na msanii Vanessa Mdee na Shaa kwani ni wasanii ambao wanajielewa na wanajitambua hivyo anatamani sana kuja kufanya nao kazi.
eatv.tv