Wanawake wa Bongo Wanalazamisha Ndoa – Dudu Baya
Msanii Dudu Baya amesema wanawake wa Tanzania wana kawaida ya kulazimisha ndoa, hasa wanapopata ujauzito hata kama ni kwa bahati mbaya.
Dudu Baya ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East africa Television, na kusema kwamba jambo hilo haliingii akilini kwani walipokutana hawakukubaliana kuona.
“Mimi mwanamke wangu ni bapa, wanawake wa kitanzania ukishampa mimba ndo kashalazimisha ndoa, suala la ndoa ni makubaliano na kama ukimuacha ndo anaenda kukupiga misumari”, amesema Dudu Baya.
Pia Dudu Baya amesema kwa sasa anatamani angeoa, kwani tayari ana watoto ambao wengine ni wakubwa.
EATV.TV