Wasanii wa Hip Hop Hatuna Hela – Young Killer
Msanii wa Hip Hop nchini Young Killer amesema sababu zinazopelekea wasanii wa hip hop nchini kutokuwa na bifu ni kutokana na mafanikio madogo wanayoyapata kupitia muziki.
Akiongea kupitia eNewz Killer amesema hakuna msanii wa hip hop mwenye mafanikio ya kupata show ya milioni 10 hivyo wanakosa cha kujitambia na ukizingatia bifu nyingi husababishwa na mafanikio makubwa japo bifu zao zipo moyoni.
Pia Killer amesema muziki wa sasa una changamoto nyingi na ili upate nafasi ni lazima uzungumziwe hivyo haoni tatizo la Young D kutupiwa dongo na Stamina kuwa hata mapaka kwa sasa wana’rap’.
Killer pia amesema anajipanga kurudi na kurekebisha kila kitu ambacho hakipo sawa.
eatv.tv