Zikiwa zimebaki siku 33 kutolewa kwa Tuzo za EATV ambazo zinahusisha wasanii wa muziki pamoja na wasanii wa filamu nchini, East Africa Television leo imetangaza wasanii ambao wamefanikiwa kuingia katika baadhi ya vipengele vya tuzo hizo.
Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Dominican Mkama, Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar es Salaam kutoka Vodacom amewataja wasanii watano wanaowania kipengele cha ‘Muigizaji Bora wa Kiume’ na wanamuziki watano wanaowania kipengele cha “Mwanamuziki Bora Chipukizi”
MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Nominee: Saidi Ally filamu aliyoigiza (Ndugu wa mume)
Nominee: Meya Shabani Hamisi filamu aliyoigiza (Facebook profile)
Nominee: Salim Ahmed (Gabo) filamu aliyoigiza (Safari ya Gwalu)
Nominee: Dotto Husein Matotola filamu aliyoigiza (Likwacha lala)
Nominee: Daudi Michael Tairo filamu aliyoigiza (Mfadhili wangu)
MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Nominee: Amani Hamisi (Man Fongo); Wimbo – Haina Ushemeji
Nominee: Feza Kessy; Wimbo – Sanuka
Nominee: Rukia Jumbe (Rucky baby) ; Wimbo – Give Me Some More
Nominee: Mayunga Nalimi (Mayunga) ; Wimbo – Nice Couple
Nominee: Rashid Said (Bright) ; Wimbo – Nitunze
Zoezi la kutaja wasanii waliofanikiwa kushiriki katika tuzo za EATV (EATV AWARDS) litakuwa ni la siku nne kuanzia leo Jumanne hadi siku ya Ijumaa baada ya hapo zoezi litarudi kwa mashabiki na wananchi kwa ajili ya kuanza kupiga kura kwa wasanii ambao wanashiriki katika tuzo.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Desemba 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Comments
comments