Artists News in Tanzania

Wastara Aeleza Sababu ya Kumpiga Kofi la Kweli Diana Ndani ya ‘FAULO’

Staa wa Bongo Movies, Wastara Juma, alimpiga kofi la kweli mwanadada Diana Kimaro, ambalo mpaka lilitoa chozi Diana wakiwa na wanaigiza filamu ya FAULO.

wastara89

Wastara

Lakini hata hivyo baada ya kumaliza kuigiza filamu hiyo, aliamua kumuomba msamaha kwa kumpiga kofi hilo ambalo lilimtoka kwa hasira.
Wastara anasema alijikuta akimpiga kofi hilo kwakuwa aliigiza kama mwanaye, akajikuta hisia za mzazi kukosewa na mtoto wake ndio kilichomfanya ampige kofi.

Alisema hata baada ya kumaliza kushot kipande hicho, baadhi ya wasanii wenzake walimuuliza kwamba anaoenekana mkali kwenye familia yake jambo ambalo alilikubali kwakuwa hana masihara na mtoto wake anapokosea.

Diana Kimaro

Filamu ya hiyo ya FAULO itasambazwa na kampuni ya Step Entertainment na itatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Comments

comments

Exit mobile version