-->

Watu 50 wauawa, 200 wajeruhiwa Las Vegas

Zaidi ya watu 50 wameuawa huku takriban watu 200 wakijeruhiwa katika tukio la ufyatulianaji risasi kwenye tamasha mjini Las Vegas.

Mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 64 akiwa amejihami kwa bunduki na mkazi wa Stephen Paddock, alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay akielekeza mtutu kwenye ukumbi wa wazi lilikokuwa likifanyika tamasha hilo.

Baadaye naye alipigwa risasi na maofisa wa polisi katika hoteli hiyo ambako ilikutwa idadi kadhaa ya silaha. Shambulio hilo linatajwa kuwa baya zaidi katika historia ya hivi karibuni nchini Marekani.

Ofisa polisi, Joe Lombardo amesema shambulio hilo lilifanywa na mtu mmoja. Aliongeza kuwa polisi walikuwa na uhakika juu ya mwanamke mmoja waliyemshuku, mapema akiitwa Marilou Danley, kwamba alikuwa amebeba silaha kabla ya shambulio kufanyika.

Ofisa huyo alisema mshambuliaji aliyekuwa amesimama katika ghorofa ya 32 ya hoteli hiyo naye aliuawa.

Hadi mchana huu Lombardo alisema hakuna katika nafasi ya kutoa maelezo ya watu waliokufa na waliojeruhiwa, lakini alithibitisha kwamba maofisa wawili wa polisi ambao walikuwa zamu ni miongoni mwa waliouawa.

Msemaji wa hospitali moja jirani ambako majeruhi walipelekwa kwa matibabu amesema watu 14 kati ya waliojeruhiwa hali zao ni mbaya.

Mashuhuda wamesema mshambuliaji alirusha risasi nyingi sana na kwa mlio wa bunduki mfululizo inaonekana alitumia bunduki inayopiga mfululizo. Mamia ya watu walikimbia eneo hilo kujiokoa.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364