WCB Wamzawadia Raymond Gari Jipya Kwenye Birthday Yake
Uongozi wa WCB umeendelea kumwaga zawadi ya magari kwa wasanii wake na sasa bahati imemuangukia Raymond.
Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii Raymond, uongozi wa WCB ukaamua kumfanyia sherehe msanii wao huyo kwenye ikulu ya Diamond iliyopo huko Madale lakini kubwa zaidi ni zawadi ya gari aliyopewa kwenye sherehe hiyo. Bosi wake, Diamond, ameweka kipande cha video kinachoonesha msanii huyo akikabidhiwa gari hilo aina ya Rav4 yenye rangi nyeusi.
“Nimeamini Mungu hana upendeleo. Nilikuwa mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani minne, nilikuwa nikihangaika na muziki wangu lakini nakushukuru sana sana kaka lao Diamond Platnumz umenifundisha vitu vingi sana hadi leo naiona njia, Boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka umenijua, umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja”. Aliandika Raymond
Mbali na hilo Raymond aliendelea kutoa shukrani kwa viongozi wake wengine huku akisema kwa mafanikio aliyopata sasa anaamini Madee anafurahia maana anajua jinsi gani ambavyo amehangaika na muziki.
“Asante sana Boss Sallam Sk kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu, nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha mengi kwenye muziki. Made Ali sitoacha kukushukuru kaka lao wewe ni kioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua sana”. Aliongeza Raymond
Raymond ameandika maneno hayo wakati akitoa maneno ya pongezi na shukrani kwa uongozi wake mzima wa WCB Wasafi kutokana na namna walivyoweza kumbadilisha na kumpigania mpaka leo hii maisha yake yamebadilika na kufanya vizuri katika muziki ambao awali alishaukatia tamaa nao.