Wema Aalikwa Kwenye 40 ya Prince Nillan Jumamosi
Kupitia kipindi cha LEO TENA kinachorushwa na CloudsFM Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zari, wamefunguka kumpa mwaliko staa wa bongo movie na mpenzi wa zamani wa Diamond,Wema Sepetu kwenye arobaini ya Mtoto wao Prince Nillan.
“Namuomba Mungu Wema sepetu amalize tatizo lake salama na yeye tumemualika kwenye shughuli ya Prince NIllan Jumamosi, itakuwa ni siku ya kipekee kabisa kuanzia asubuhi na watakaofika ni wale wenye kadi za mialiko tu”-Diamond
Sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Februari 11 mwaka huu huko kwenye ikulu ya Diamond na Zari iliyopo Madale.