Wema Sepetu Afungukia Kutajwa kwenye Nyimbo ya Bongo Fleva
Mlimbwende Wema Sepetu ambaye wengi humuita msanii mwenye nyota yake, amesema watu wanamfanyia vitu vya ajabu ili kujinufaisha likija suala la kuimba muziki, kwani kwake jambo hilo limeshindikana kabisa.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Wema amesema yeye hana mpango wa kuingia kwenye muziki, na hata wimbo wa Haitham alioshirikishwa hakuimba, lakini wamemgeuka na kuandika kwamba ameshirikishwa kuimba kwenye wimbo huo.
“Mi kuimba siwezi mwenzangu, kila nikijaribisha inabuma, ile nyimbo na Haitham umeshanisikia naipush, mi nafanyaga nilivyofanya halafau watu wananifanyia vitu vya ajabu, wananisaliti”, amesema Wema Sepetu.
Hivi karibuni msanii Haitham ameachia wimbo unaoitwa Play boy huku ukiandikwa ameshirikishwa Wema Sepetu, lakini hakuna mahali ambapo msanii huyo amesikika kuimba wala kurap na kuibua maswali mengi kwa wadau kwanini imekuwa hivyo.