Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28).
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Msanii huyo ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.
Comments
comments