Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ameshindwa kujizuia kwa kuonesha uchungu alioupata baada ya kusikia taarifa za msiba wa aliyekuwa mwanaume wa Zari ‘Ivan Semwanga’ na kumfariji mzazi mwenzake na marehemu Zari The Boss Lady.
Wema Sepetu amesema ameumizwa na taarifa hizo huku akiwaonea huruma watoto wa marehemu ambao amewaacha wakiwa wadogo.
“Broken hearted??? Rest In Peace Ivan SHOCKING NEWS kwakweli… My Condolences to The whole Family… Mungu awatie nguvu wale watoto jamani… ? They are too young… And Mungu amtie nguvu Mama watoto wako… It will be a very hard period of time for all of you But it shall pass”,ameandika Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Marehemu ‘Ivan Semwanga’ amefariki jana usiku kwa maradhi ya Shambulio la Moyo na ameacha watoto watatu wote amezaa na mrembo Zari ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Msanii wa Bongo Fleva Diamond Patnumz.
By Godfrey Mgallah
Bongo5
Comments
comments