SIMBA! Kufuatia lile sakata la jina la mnyama Simba ambapo Diamond amekuwa akijiita jina hilo siku za hivi karibuni na msanii Mr Blue kudai kuwa alilianzisha yeye kujiita simba huku mkongwe Afande Sele akisisitiza yeye ndiyo samba dume, mastaa wengi wa hapa bongo wamekuwa wakijiita majina ya wanyama ikiwa ni namna moja ya kuchombeza sakata hilo wakati msanii Alikiba akijiita kuwa yeye ndiyo balozi wa wanyama wote.
Naye staa wa Bongo Movies Wema sepetu hakuwa nyuma kwenye kuchombeza sakata hilo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandiaka;
“Watu walikuwa wanasubiria na mimi nitaje jina langu la mnyama… Mi ni Mnyama Ndio na Jina Langu ni WEMA SEPETU…. Gnyt Y’all…. Langu mwenyewe hilo…. Ila Balozi Kasema…. hihihihihi,” ameandika Wema.
Wengi memeona kuwa hilo ni dongo kwa wasanii wote wanaogombania jina la mnyama Simba akiwemo Diamond na kumsifia msanii Ali Kiba ambaye alijiita yeye ni balozi wanyawa wote kwa kuwa yeye ni moja kati ya mabalozi wa shirika la Wild Aid, shirika linalopigania haki za wanyama.
Comments
comments