Staa na mrembo kutoka Bongo Movie, Wema Sepetu na shosti wake wa karibu Muna kimenuka – Kupitia mtandao wa Instagram Wema Sepetu amemtuhumu rafiki yake huyo kumtumia mama yake kama ‘ndondocha’.
Kupitia mtandao huo, Wema ameandika:
Rose Alphonce Nungu… Nakuita tena kwa mara ya pili Rose Alphonce Nungu…. Unanitafutia nini wewe mwanamke…!? Nini nimekukosea wewe dada…? Niliapa na Miungu yote siwezi kupost kitu chochote kwa account yangu kinachokuhusu wewe ila wallahy wewe dada You are pushing my buttons… Tena una push buttons zangu kikweli kweli cuz nimekaa kimya na yako mengi…. Usijisahaulishe leo nimekuja kwako na ukalia mno kutaka vitu visitoke kwenye mitandao… Sasa nakwambiaje Rose, mimi sitovitoa mitandaoni cuz im nat dat illiterate kama wewe… But nataka kukuuliza kitu, kwanini unamfanya mama angu kama ndondocha wako…? Let me tell u one thing, Rose, I have been in the industry kwa miaka 10, Never have I taken my mum kwenye sehemu za starehe tena usiku wa manane… Ntamuita mama angu pale ninapojua kuwa uwepo wa mam unahitajika kwenye hafla hii… Umekuja ukaamua kujiweka karibu na mama angu kiasi cha kwamba mimi tena nikawa sio shoga ako bali mama angu ndo ukamtawala…. Ulikuwa una yako… Leo hii umeweza kumteka mama angu kiasi cha kwamba unamfanya ajione yuko age sawa na wewe… Mama angu ni wa kwenda mango garden jamani? sijawahi… Mama angu ni wa kukaa mpaka usiku wa manane kwenye wanja za starehe? Sijawahi.. Mama angu leo hii ni wa kumlisha maneno ya uongo na kweli akaonekana mbele ya binaadam ananikana mtoto wake wa kumzaa…? Muna ulichomfanya mama angu Mungu ndo anajua na ipo siku isio na jina basi atakuadhirisha ila kaa ukitambua watoto wake wote hatupendi… So back to topic ya leo, umeona uendeleze ushenzi wako kwa kuanza kutunga uongo kwa watu wangu wa karibu… kama ulivyotangaza kwenye magroup yako kuwa unanipa mabwana… Hivi Rose, mimi leo hii wewe unitaftie bwana kwakuwa wewe hutaki mabwana wa maana… Honey mimi sitafutiwagwi bwana… Mabwana wananitongoza wenyewe na mara nyingi nakuwa na mtu ninaempenda sio niliotafutiwa… Mimi sio mtoto mdogo… Sasa naona umeanza na @junaithar kesho na kesho kutwa usiwasahau @directorjoan na @sweetlorah … Afadhali hawa dada zangu naweza kuwapostia hata biashara zao na wakanilipa … Niambie nini umefanya kwangu wewe.. Umenidhulumu vingapi nimekaa kimya… Niseme…? i
Comments
comments