Msanii Wema Sepetu leo amefika Mahakamani kufuatilia kesi yake ya kukutwa na msokoto wa Dawa za Kulevya aina ya Bangi
Wema amefika Mahakamani hapo akiwa na Wakili Albert Msando aliyetangaza kumtetea baada ya Wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea msanii huyo
mrembo Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa leo February 8, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille ameieleza Mahakama kuwa hakuwepo wakati Wemaakichukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali.
Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando.
Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, amedai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Inspekta Wille amedai kuwa February 8, 2017 alifika katika Ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali saa 5 asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo wa Wema.
Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille kama alikuwepo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki unachukuliwa ambapo alijibu kuwa hakuwapo.
Msando alimuhoji Inspekta Wille kuwa walikaa kwa muda gani katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Inspekta Wille alidai kuwa hakumbuki.
Katika maelezo yake, pia Inspekta Wille amedai yeye hakupekuwa katika chumba anacholala Wema bali alipekuwa katika chumba anachohifadhia nguo na viatu.
Amedai kuwa katika upekuzi walikuta msokoto wa bangi jikoni juu ya kabati, pia walikuta msokoto wa bangi uliotumika ukiwa ndani ya kiberiti dirishani katika chumba wanacholala wafanyakazi wa Wawili wa Wema.
Baada ya kueleza hayo, aliiomba Mahakama ipokee hati ya ukamataji mali iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Wema kama kielelezo.
Kesi imeahirishwa hadi February 26 na 27, 2018 itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Comments
comments